truck
Free Shipping

Delivered Electronically

phone
+254 (0) 718 989 058

Call us now

Diwani ya Tamasha

Sold by: Dr. Aggrey Wanyama

Social

5 5 4 Product

Price

$4.37 (450.00 KES) each

Brand

Brand : Gateway Publishers
+

eSomeni

Where Authors Meet Readers

Tajiriba ya miaka mingi ya kuandaa wanafunzi kwa mitihani ya kitaifa katika kiwango cha shule za upili imenifunza kuwa si wengi ambao hushabikia maswali ya ushairi katika mitihani.Wengi wamejazwa kasumba potofu kuwa ushairi ni utanzu mgumu.Jambo hili limeniatua moyo kwani kulingana nami,huu ndio utanzu mwepesi zaidi ambao kwao,mtahiniwa anaweza kukwangura alama za juu zaidi.Hii ndiyo imekuwa sababu kubwa ya kuandika kitabu hiki ili,japo kwa njia finyu,kichangie katika kuimarisha matokeo ya wanafunzi kwenye kitengo cha ushairi.
Aidha,baada ya kutunga mashairi na kuyatumia katika tamasha za drama na muziki kwa muda mrefu,nilihisi kuwa kazi hii ingetumiwa katika kufikia watu wengi zaidi kama ingetungiwa kitabu.Ni kwa misingi hii ndiposa nimependekeza kazi hii iitwe Diwani ya Tamasha.Kwangu,hii itakuwa heshima kubwa kwa wanafunzi wa Nyamagwa Boys ambao kwa miaka kumi na mitatu niliyokuwa nao,hamna mwaka hata mmoja ambao tulikosa kuwakilisha Mkoa
wa Nyanza katika tamasha za muziki – kiwango cha kitaifa.Isitoshe,kazi hii ni dhihirisho tosha kuwa kizaliwacho huwa kizuri zaidi kuliko kinachozaa.Shairi kwa anwani ukware lilitungwa na malenga mwendazake Hesborn Nyairo (Mungu amweke mahali pema) aliyeinukia kuwa mmoja kati ya wanafunzi wangu maarufu zaidi.Shairi hili liko katika diwani hii kama kumbukizi kwa heshima yake.
Katika kazi hii, imeonelewa kuwa ni bora kuangazia aina za maswali ambayo aghalabu hutokea katika mitihani ya kitaifa.Licha ya haya, maelezo mafupi kuhusu mambo muhimu yanayohitajika ili kulikabili barabara kila aina ya swali yametolewa.Baada ya kufanya haya yote, kuna mashairi yaliyotungiwa maswali mahsusi na majibu yao.Kwa njia hii ndogo, tunashawishika kuwa watahiniwa watanufaika pakubwa.
List of the comments:
No comments have been posted yet.
Vote:

Give your advice about this item:

Username:
E-mail:

From our Blog

  • Do You Avoid Reading Ebooks? By Remez Sasson Do you read ebooks, or avoid reading them? Does it seem to you awkward and inconvenient to read ebooks on the screen? Well, this depends on what…